BAADA ya kuondolewa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika,
Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm,
amesema kuwa nguvu zao zote wanazielekeza kwenye
Ligi Kuu Bara wakati timu yao ikianza kucheza na African
Lyon.
Yanga iliondolewa kwenye michuano hiyo ikiwa ya mwisho
 katika kundi lao ikiwa na pointi nne huku TP Mazembe
wakiongoza wakiwa na 13.
Timu hiyo, inatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza ya
 ligi kuu Jumapili hii kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar
es Salaam dhidi ya African Lyon iliyopanda daraja msimu
uliopita.

Pluijm alisema amefanya kikao na wachezaji wake mara
baada ya mechi na Mazembe kumalizika kwa timu yake
kufungwa mabao 3-1 na kikubwa amewataka kusahau
yaliyopita na badala yake wahamishie nguvu kwenye
ligi kuu.
Pluijm alisema, kupitia michuano hiyo, wamejifunza
mengi ikiwemo mbinu za wapinzani wao pamoja na
kupata uzoefu akiamini mwakani watafikia katika
hatua nzuri.
Aliongeza kuwa, amefurahishwa na morali kubwa ya
wachezaji wake baada ya kutolewa katika michuano
hiyo, hivyo wameahidi kulitetea taji lao la ubingwa
katika msimu huu.
“Kikubwa ninapenda kuwapongeza wachezaji wangu
 kupambana katika Kombe la Shirikisho Afrika, licha
ya kutolewa katika hatua ya Nane Bora inayoshirikisha
 timu nane bora Afrika.
“Mara baada ya kumaliza mechi ya mwisho na Mazembe,
 nilifanya kikao na wachezaji kwa ajili ya kuwatengeneza
kisaikolojia ili tutakaporejea kwenye ligi kuu turudi na
nguvu zote katika kulitetea taji hilo.
“Hivyo, hatutataka masihara wala kudharau timu yoyote
 inayoshiriki ligi kuu zikiwemo zilizopanda daraja tuhakikishe tunautetea ubingwa wetu tunaoshilikia,” alisema Pluijm.

Post a Comment

 
Top