KOCHA Mkuu
wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amepanga kurejesha imani na furaha
iliyopotea kwa mashabiki wa timu hiyo kwa kuhakikisha wanawafunga MO Bejaia
kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Timu hiyo
iliyopo mkiani katika Kundi A, ikiwa na pointi moja, imepoteza michezo mitatu
na kutoka sare mmoja kati ya michezo minne iliyocheza.
Hata hivyo,
kipigo kilichoshtua zaidi ni cha mabao 3-1 ilichokipata dhidi ya Medeama, hivi
karibuni.
Yanga
inatarajiwa kuvaana na MO Bejaia Agosti 13, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wake wa tano.
Pluijm
alisema matokeo mabaya wanayoendelea kuyapata yanawakatisha tamaa mashabiki na
kusababisha imani na timu yao kupungua.
"Tupo
'serious' hivi sasa katika maandalizi ya mechi yetu na MO Bejaia ambayo siyo
ndogo kwetu, licha ya ugumu uliopo, lakini tutapambana kuhakikisha tunawafunga
MO Bejaia.
"Ninajua
imani ya mashabiki imepotea kwa kiasi kikubwa, hivyo nilichopanga ni kuirejesha
kwa kuifunga MO Bejaia hapa nyumbani ili watoke uwanjani nao wakifurahia.
"Hilo
linawezekana na nitahakikisha mashabiki wa timu hii wanakuwa na furaha,
nimeshazungumza na wachezaji wangu na kuwaambia kuwa tunatakiwa kuwapa furaha
mashabiki,” alisema Pluijm.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.