STRAIKA wa
Simba, Ibrahim Ajib, jana asubuhi kwenye mazoezi ya timu hiyo alijikuta akiliwa
Sh elfu kumi bila ya kutarajia baada ya kuwekeana dau na kipa wa timu hiyo,
Denis Richard.
Ishu ilikuwa
hivi; Baada ya kumalizika kwa mazoezi ya asubuhi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa
Highlands mkoani hapa ambapo Simba imepiga kambi, Ajib alikuwa akisema katika
penalti tano atakazompigia Denis, basi hadaki hata moja na kama akidaka japo
moja basi atampa kiasi hicho cha fedha.
Championi
ambalo lilikuwepo uwanjani hapo, lilishuhudia kila kitu mwanzo hadi mwisho
ambapo muafaka ulifikiwa kwamba Ajib apige penalti hizo na Denis akakae
langoni, jambo ambalo lilikubaliwa na kila mmoja huku wachezaji wakiwa na
shauku ya kuona nini kitatokea.
Cha
kushangaza na kufurahisha ni kwamba, penalti ya kwanza tu Denis akaiokoa, hivyo
mchezo ukaishia hapo ambapo baada ya kuiokoa wachezaji wenzake wakamshangilia
kwa nguvu huku wengine wakimbeba kutokana na kuonyesha umahiri wake wa kudaka
penalti.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.