![]() |
Angban |
KIPA namba moja wa Simba, Muivory
Coast, Vincent Angban, ametamka kuwa kuja kwa kipa mwingine ndani ya timu hiyo,
Mwadini Ali kutampa changamoto ya namba mara baada ya kukosa upinzani mbele ya
kipa mwenzake Peter Manyika jambo ambalo lilimfanya kutumika yeye kwenye sehemu
kubwa ya msimu uliopita.
Viongozi wa Simba wamemjumuisha
Mwadini Ali kutoka Azam katika kikosi chao cha msimu ujao ambapo kipa huyo
ametua sambamba na mshambuliaji Ame Ali ‘Zungu’ ambapo wote wapo kwa mkopo.
Angban amesema kuwa hana shaka yoyote
na ujio wa Mwadini katika kikosi hicho kwa kuamini kuwa atamfanya kiwango chake
kikue zaidi ya msimu uliopita.
![]() |
Mwadini |
“Kuja kwake Mwadini hapa Simba ni
jambo zuri kwetu kwa sababu tumezidi kuwa makipa wengi wenye viwango vikubwa
pamoja na uzoefu na jambo hilo naamini litatusaidia kuifanya timu ipate
mafanikio zaidi.
“Lakini kwangu pia naamini atanipa
msaada wa kuinua kiwango changu kwa sababu mwanzo nilikosa mpinzani halisi
lakini kwa hapa nitakuwa makini kwa kuonyesha uwezo kwani najua nisipofanya
hivyo yeye atajituma na kuchukua namba yangu,” alisema Angban.
Post a Comment