KOCHA wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali, amepata
pigo kufuatia kufiwa na baba yake mzazi, mzee Fakehe Juma aliyekuwa akiishi
mkoani Tanga.
Pondamali alikuwa nje ya nchi wakati msiba huo
unatokea wakati timu yake ya Yanga ilipokuwa ikicheza na Medeama ya Ghana
katika mchezo wa marudiano na kujikuta ikichapwa mabao 3-1.
Pondamali ameeleza kuwa, alipigiwa simu alipokuwa
Ghana kufahamishwa juu ya msiba wa mzazi wake huyo, hivyo ilimlazimu kwenda
kuhani mara tu baada ya kuwasili Bongo.
“Kwa sasa mimi sipo na timu kwa kuwa nipo Tanga
kuja kuhani msiba wa baba yangu mzazi mzee Juma wakati nipo Ghana, hivyo nilivyofika
airport nilipitiliza moja kwa moja hadi huku.
“Ni pigo nililolipata ila namshukuru Mungu kwani
ndiye muweza wa yote, natarajia kuwasili Dar wiki ijayo ili kuendelea na
mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya MO Bejaia na kwa upande
wa makipa wangu wako fiti,” alisema Pondamali.
Post a Comment