EDWARD
Lowassa jana aliibukia kwenye Mkutano Mkuu wa Simba, hakufika kwa umbo lakini
staili yake ilifika. Unaikumbuka ile staili ya ushangiliaji iliyokuwa inatumiwa
na mgombea huyo wa urais katika uchaguzi uliopita kupitia Chadema kwa mwamvuli
wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)? Basi aina yake ya ushangiliaji iliteka
mkutano huo.
Simba walifanya mkutano wao huo jana kwenye Ukumbi wa Bwalo la
Polisi, Masaki jijini Dar es Salaam uliohudhuriwa na wanachama 700.
Katika
mkutano huo uliokuwa wa vituko na vioja vingi kutoka kwa wanachama hao,
walikubaliana kupitisha ajenda kumi ambazo zote zilipitishwa chini ya Rais,
Evans Aveva.
Lakini
kabla hata mkutano haujaanza watu walionekana wanataka mabadiliko. Mkutano huo
ulianza saa 5:08 asubuhi huku baadhi ya wanachama wakionekana kutaka mabadiliko
ya mfumo wa uendeshaji wa timu hiyo.
Dalili
hizo za wanachama hao kutaka mabadiliko zilianza mapema kabla ya rais wa timu
hiyo kuanza kupitia ajenda pale alipotoa salamu kwa kutamka Simba na wenyewe
wanachama wakatamka mabadilikoo, huku wakiichezesha mikono yao kama ile staili
ya mabadiliko iliyoanzishwa na Ukawa baada ya kumpata Lowassa.
Lowassa
alivuma sana kwa staili hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika
Oktoba, mwaka jana. Lilipokuwa likitamkwa jina lake Lowassaaaa, watu waliitikia
mabadilikooo, ilipotamkwa mabadilikooo, waliitikia Lowassaaa. Sasa jana ilikuwa
ni “Simbaaa” halafu watu wanaitikia mabadilikooo.”
Kimsingi,
wanachama karibu wote waliohudhuria mkutano huo wa jana, walitaka timu hiyo
apewe Mohammed Dewji, maarufu kwa jina la Mo ambaye anataka kununua hisa 51 za
klabu hiyo kwa dau la Sh bilioni 20.
Kitendo
hicho cha staili ya Lowassa hakikutokea kwa Aveva pekee, pia ilitokea kwa Mwakilishi
wa TFF, Wallace Karia aliyepita mbele na akatoa salamu kwa kutamka Simbaaa na
wanachama wakaitikia mabadilikooo.
Hali
hiyo, ilikuwa ikitokea kila wakati pale wanachama au viongozi wakipita mbele ya
ukumbi kwa ajili ya kutoa salamu ya kutamka Simba badala ya kuitikia oyeee,
wanachama wakawa wanatamka mabadilikooo.
Aina
hiyo ya ushangiliaji iliendelea hadi mwisho wa mkutano huo saa 7:00 mchana mara
baada ya Aveva kufunga mkutano huo.
Post a Comment