MJUMBE wa
ngazi ya juu wa Kamati ya Olimpiki, Patrick Hickey amewekwa chini ya ulinzi kwa
kuhusishwa na ufisadi wa tiketi za Olimpiki.
Afisa huyo
amejiuzulu kwa muda ili kupisha uchunguzi baada ya kuwekwa chini ya ulinzi kwa
kuuza tiketi kinyume cha sheria.
Kumekuwa na
uhudhuriaji mdogo katika michezo ya olimpic huko Rio ni kutokana na tiketi
kuuzwa na baadhi ya maafsa kwa bei ya juu sana kimagendo.
Kukamatwa
kwa Patrick Hickey, mmoja wa viongozi wa juu wa michezo ya Olympiki ya Ulaya,
bado ni hoja kubwa kwa makao makuu ya polisi ya Brazil, kufuatia kukwamatwa kwa
viongozi hao kumehusishwa kampuni ya kimataifa ya usimamizi wa michezo, THG.
Zaidi ya
tiketi elfu moja za michezo ya olimpiki zimesitishwa, ikiwemo tiketi za
ufunguzi na zile za mbio za riadha, na wachunguzi wanasema madai ya udanganyifu
yangeweza kutengeneza zaidi euro milioni mbili.
Kampuni hiyo
ya kusimamia michezo ya kimataifa imekanusha shutma hizo huku jaji wa Brazil
wiki hii akitoa agizo la kukamatwa washukiwa zaidi waliohusika na kesi hiyo.
CHANZO: BBC
Post a Comment