Bingwa wa
mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji kutoka Kenya Ezekiel Kemboi
amenyang'anywa medali yake ya shaba aliyoishinda mjini Rio de Janeiro, Brazil.
Kemboi, 34,
aliyemaliza wa tatu katika mbio hizo, alikuwa amepewa nishani ya shaba.
Lakini
Ufaransa ilikataa rufaa baada ya kubainika kwamba mwanariadha huyo wakati
mmoja, baada ya kuruka kiunzi na maji, alikanyaga nje ya mstari wakati
akishiriki mbio hizo Jumatano.
Mfaransa
Mahiedine Mekhissi, aliyemaliza nafasi ya nne, amepandishwa hadi nafasi ya tatu
na kupewa nishani ya shaba.
Kemboi,
aliyeshinda Olimpiki za London 2012 katika michezo ambayo Mahiedine
Mekhissi-Benabbad alishinda fedha, tayari ametangaza kwamba atastaafu.
Mshindi wa
mbio hizo za Rio alikuwa Mkenya Conseslus Kipruto ambaye pia aliweka rekodi
mpya ya Olimpiki , muda wake ukiwa 8:03.28.
Mmarekani
Evan Jager alimaliza wa pili muda wake ukiwa 8:04.28.
Muda wa
Kemboi ulikuwa 8:08.47 na wa Mekhissi 8:11.52.
CHANZO: BBC
Post a Comment