Saa chache
baada ya Rais wa Simba, Evans Aveva kushikiliwa na Taasisi ya Kupambana na
Kuzuia Rushwa (Takukuru), kumeibuka sababu kadhaa ambazo zinazungumzwa kuwa ni
chanzo.
Taarifa
zinaelezwa kuwa Takukuru wanamshikilia Aveva kwa tuhuma za rushwa ingawa
haijaelezwa ni tuhuma zipi.
Kumekuwa na
taarifa ambazo si rasmi kuwa Aveva aliingiza fedha za Okwi zaidi ya Sh milioni
450 kwenye akaunti yake binafsi kuhofia zichukuliwe na TRA kwa kuwa Simba
inadaiwa.
Simba
inadaiwa zaidi ya Sh milioni 650, hali hiyo imesababisha kuonekana kama vile
alikuwa akikwepa kodi.
Malipo ya
fedha hizo, zaidi ya Sh milioni 450 ni malipo ya ununuzi wa mshambuliaji
Emmanuel Okwi ambazo Simba ilimuuza katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
Taarifa hizo
zimeeleza kwamba waliamua kuzificha ili waweze kujenga uwanja wao wa Bunju
ambao tayari walianza kuujenga
Lakini kuna
baadhi wamekuwa wakieleza kwamba Aveva ana kisa na mtu nje ya hapo ambaye
‘amemchoma’.
Hata hivyo,
kwa kuwa Takukuru bado wanaendelea na uchunguzi na suala lake ni tuhuma,
uchunguzi utakapokamilika, wao ndiyo wataeleza ukweli tupu kuhusiana na suala
hilo.
Salehjembe
Post a Comment