KIPA wa
Yanga Ali Mustapha 'Barthez', leo amefanya mazoezi ya ndani na wachezaji
wenzake wa kikosi hicho tofauti na yale ya kulinda lango.
Barthez
aliamua kufanya mazoezi hayo mepesi ya ndani huku akionekana kumudu kutoa pasi mara
kadhaa wenzake, ili kujiweka fiti zaidi kutokana na kutocheza kwa muda mrefu
mechi za kiushindani za kimataifa kutokana na mara nyingi Kocha Hans van Der
Pluijm kumtumia Dida.
Pia kipa wa
zamani wa Simba, Juma Kaseja akiwa na kikosi hicho cha Msimbazi aliwahi kufanya
mazoezi ya ndani na kudai kuwa aina hiyo ya mazoezi huwasaidia makipa hasa anaporudishiwa
na wachezaji wake.
Yanga inajindaa
na mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MO Bejaia utakaochezwa
Julai 13, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Mshambuliaji Donald Ngoma
anatarajiwa kukosa mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi.
Post a Comment