BAADA ya kusambaa kwa picha mtandaoni zikimuonesha
mshambuliaji wa Azam Kipre Tchetche akitambulishwa na klabu ya Al Nahdha ya
Oman Uongozi wa klabu hiyo hawatambui chochote kinachoendelea.
Mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast alikuwa akihusishwa na
kujiunga na kujiunga na moja ya klabu kongwe hapa nchini kabla ya kuibukia
nchini Oman.
Mtendaji mkuu wa Azam Saad Kawemba amesema hawafahamu
chochote kuhusu kuondoka kwa mshambuliaji hiyo kwakua bado amebakiwa na mkataba
wa mwaka mmoja ndani ya wanalambalamba hao.
"Kipre bado ni mchezaji wetu halali ana mkataba wa mwaka
mmoja kama kuna timu inamuhitaji lazima waje kwetu tukae nao tumalizane,"
alisema Kawemba.
Aidha Mtendaji huyo alisema iwapo utaratibu wa kusajiliwa
hautofuatwa Azam hawatatoa nyaraka zozote kwa mshambuliaji huyo kitu
kitakochosababisha kutocheza katika timu yoyote.
"Hatutatoa nyaraka mpaka utaratibu utakapofuatwa
vinginevyo hatocheza huko aliko," alisema Kawemba.
Tangu kumalizika kwa msimu wa ligi wachezaji wa Azam
walipopewa likizo Kipre hakurudi tena Azam huku wengine wote wakifanya mazoezi
chini ya kocha Mhispania Zeben Hernandez.
BOIPLUS
Post a Comment