RAIS wa
klabu ya Simba, Evans Aveva amesema kuwa
msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ni wa kwao
katika mafanikio kwao huku akitamba kikosi chao kitakuwa tishio kama
Medeama ya Ghana.
Kauli hiyo,
aliitoa hivi karibuni mara baada ya kumaliza Mkutano na Waandishi wa Habari
kwenye Ukumbi wa Milenium Tower uliokuwepo Makumbusho Jijini Dar es Salaam.
Jeuri hiyo,
huenda akaipata zaidi mara baada ya Mfanyabishahara mkubwa nchini, Mohamed
Dewji kuahidi kuwekeza kwenye klabu hiyo ikiwemo kutoa fungu la usajili kwa
ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.
Aveva
alisema hawaoni sababu yoyote ya wao kuukosa
Ubingwa wa ligi kuu na Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na mikakati
wanayoendelea nayo ya kukiimarisha kikosi chao.
Aveva
alisema, timu yao inaendelea na kambi yao ya pamoja chini ya Mcameroon, Joseph
Omog na Mganda, Jackson kwa kuziimarisha sehemu mbalimbali, licha ya kocha wao
huyo kuwathibitishia viongozi kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya ligi.
Aliongeza
kuwa, wakati kocha huyo akiendelea kukiimarisha kikosi chake, bado anaendelea
kuwaangalia wachezaji wa kimataifa waliokuwepo kwenye majaribio hayo akiwemo
Janvier Bukungu, Mousa Ndusha (DR Kongo), Method Mwanjali (Zimbabwe) na Fedric
Blagnon raia wa Ivory Coast.
"Kama
uongozi kiukweli tumejidhatiti vya kutosha kuhakikisha mwaka huu unakuwa wa
mafanikio kwenye klabu yetu, tunashukuru jitihada hizo tayari tumezianza kwa
maana ya timu kuiweka kambi kwa muda mrefu.
"Tunajivunia
benchi zuri linaloongozwa na Omog huku akiendelea kukiaandaa kikosi chake kwa
ajili ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu ndani ya wakati mmoja akiendelea na
zoezi zima la usajili kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chetu.
"Msimu
uliopita uongozi tulishindwa kuuchukua ubingwa kutokana na matatizo ya hapa na
pale ikiwemo usaliti wa wachezaji, lakini safari hatutakubali kutokana kwani
tuna kikosi kilichokuwa imara na bora kitakacholeta ushindani wa ligi kama
Medeama ya Ghana (waliowafunga Yanga Caf),"alisema Aveva.

Post a Comment