KOCHA
wa Chelsea, Antonio Conte, amewaacha watu hoi aliposema kuwa hajui kama
mshambuliaji wa timu hiyo Diego Costa atabaki
kwenye klabu hiyo.
Costa
hakucheza mchezo wa maandalizi ya msimu walipovaana na Real Madrid na kufungwa
mabao 3-2 nchini Marekani, wikiendi iliyopita.
Inaelezwa
kuwa mchezaji huyo hakucheza mchezo huo kwa kuwa alikuwa akilalamika kuhusu
maumivu ya nyama za nyuma za miguu na hakufanya mazoezi na timu hiyo.
Chelsea
wanakaribia kumsajili Romelu Lukaku kwa kitita cha pauni milioni 60 (zaidi ya
shilingi bilioni 130) na inaonekana kuwa kama wakifanikiwa kumsajili mchezaji
huyo, basi Costa atakwenda kwenye klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid.
“Naweza
kusema kuwa leo Costa ni mchezaji wa Chelsea, hajacheza mchezo huu kwa kuwa
anaumwa.
“Lakini
najua kama akipona basi atarudi uwanjani akiwa na nguvu mpya namwamini sana,
lakini leo ndiyo nasema hivyo, ukiniuliza kesho nitakuambia sijui kama ni
mchezaji wetu hapa.
“Kwenye
timu hii kuna wachezaji ambao watabaki na wengine wataondoka, hivyo ni jambo la
kusubiri kwa kuwa sijui kama Costa atabaki.”
Post a Comment