MSHAMBULIZI wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa
Stars’ na klabu ya Yanga SC, Jerson Tegete amethibitisha kuwa ataachana na
Mwadui FC baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa mwaka mmoja.
Tegete mshindi wa mataji manne ya ligi kuu (2008/09,
2010/11, 2012/13, 2014/15) alijiunga na Mwadui ya Shinyanga mwaka mmoja
uliopita akiwa chini ya Kocha Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’.
“Ni kweli nimemaliza mkataba wangu na Mwadui. Nitaondoka
katika timu hiyo,” anasema Tegete nilipofanya naye mahojiano mafupi siku ya Jumatano
hii.
Mshambulizi huyo alicheza kwa miaka saba katika kikosi cha
Yanga na ni kati ya washambuliaji wawili waliopata kufunga magoli mengi katika
historia ya ‘Dar es Salaam derby’ sambamba na Emmanuel Gabriel waliofunga
magoli matano kila mmoja.
Msimu uliopita alifunga magoli matano tu katika VPL na kuwa
kinara wa ufungaji katika timu yake.
“Nipo katika mazungumzo na baadhi ya timu, soon nitawaambia
ni timu gani nitachezea msimu ujao. Itakuwa ni timu ya hapa nyumbani,” anasema
Tegete ambaye ni mmaliziaji aliyetajwa ‘mviziaji wa kiwango cha juu.’
Chanzo: Shafiidauda
Post a Comment