KIKOSI cha Tanzania Prisons kinachonolewa na Kocha, Salum
Mayanga kimeripotiwa kupata mrithi wa aliyekuwa kipa wao tegemeo, Beno
Kakolanya, kwa kumsainisha kipa wa zamani wa Simba na Kagera Sugar, Andrew
Ntala.
Prisons ambayo maskani yapo mkoani Mbeya tayari imewapoteza nyota wake wawili tegemeo
ambao ni Kakolanya na Mohammed Mkopi aliyetua kwa majira zao Mbeya City baada
ya mkataba wake na Wajelajela hao kumalizika.
Nyota wengine walioungana na Ntala kutia saini ni Samatta
ambaye aliwahi kucheza Mgambo Shooting.
Post a Comment