Uongozi wa Klabu ya Stand United ya Mjini Shinyanga
inayodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA umeendelea na
maandalizi ya kujiweka vizuri na msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania bara pamoja
na kombe la Shirikisho.
Baada ya usajili wa wachezaji 14 ambao niliwataarifu wiki
iliyopita,tayari kuna wachezaji wengine wameongezeka katika orodha ya wachezaji
watakaoichezea Stand United katika harakàti za kuiweka timu katika hali ya
ushindani.
Katika kujiimarisha zaidi Tumemsajili Edward Charles
anayeweza kucheza kama beki namba 3 na kiungo namba 6 kutoka katika klabu ya
Geita Gold SC ya Geita zamani aliwahi kuichezea Yanga na amesaini mkataba wa
miaka miwili.
Mchezaji wetu Abuu Ubwa amekubali kuongeza mkataba wake kwa
miaka miwili zaidi. Pia tumeweza kunasa saini za vijana vijana chini ya miaka
20 Charles Stanslaus kutokea Serengeti Boys, David Mwita na Ganga Migele
(Shinyanga), Salum Kijibwa na Paul Barama (wametokea Gormahia ya Kenya), Kareem
Sadick (Police Mara).
Kambi rasmi ya Stand United inatarajiwa kuanza siku ya
Junamosi jijinì Dar esa Salaam
Imetolewa na
ALEXANDER SANGA
MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO
STAND UNITED COMPANY LIMITED
0715052491
Post a Comment