KIPA Juan Jesus Gonzalez  amewasili jana nchini kutoka Hispania kujaribu kujiunga na mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC.
Kipa huyo amepokewa na Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga jana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam tayari kwa majaribio.
Katika hatua nyingine, jopo la makocha sita kutoka liliwasili juzi Dar es Salaam kuanza maandalizi ya msimu ujao wa 2016-2017).
Hao ni Kocha Mkuu Zeben Hernandez, Msaidizi wake Yeray Romero, Kocha Mkuu wa Viungo Jonas Garcia, Msaidizi wake, Pablo Borges na kocha wa Makipa Jose Garcia.
Jopo hilo la makocha litaongezewa nguvu na makocha wengine wazawa waliokuwa na Azam FC msimu uliopita, Kocha Msaidizi Dennis Kitambi na wa Makipa, Idd Abubakar.
Aidha, Daktari mpya wa timu hiyo, Sergio Perez, anatarajia kutua nchini Julai 12 mwaka huu kutoka Hispania pia
Makocha hao wanatua nchini kuziba nafasi za benchi la ufundi lililopita la Azam FC chini ya Stewart Hall, Msaidizi wake Mario Marinica na Mtaalamu wa Viungo, Adrian Dobre, waliojiuzulu kuinoa timu hiyo mara baada ya mchezo dhidi ya JKT Ruvu (2-2) msimu uliopita.
chanzo: binzubery

Post a Comment

 
Top