KAMA
mambo yakienda sawa, katika mchezo wa leo Jumamosi dhidi ya Medeama SC ya
Ghana, mipira ya krosi, faulo na kona ya Yanga mingi itakuwa inachezwa na Obrey
Chirwa.
Na kama Chirwa akiwa pembeni mbali na lango la adui,
basi kazi hiyo itafanywa na Donald Ngoma au Amissi Tambwe, lengo ni kuifunga
Medeama.
Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm katika mazoezi ya
jana asubuhi alikuwa akimpa maelekezo maalum Chirwa juu ya namna ya kuunganisha
mipira ya krosi, kona na faulo jirani na lango la adui.
Yanga leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
inacheza na Medeama ya Ghana mechi ya Kundi A ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mbali na hilo, Pluijm katika mazoezi ya jana alionekana
akimkomalia Chirwa kwa kumpa ufundi wa jinsi ya kuwaibia mabeki na kuiwahi
mipira ya krosi za kutanguliziwa ama faulo fupi ili afunge.
Katika mazoezi hayo, Pluijm alionekana kuwa mkali
akihimiza krosi nyingi kutoka wingi ya kulia chini ya Simon Msuva na Chirwa
kwenye wingi ya kushoto.
Kuna uwezekano mkubwa leo Pluijm akawaanzisha
washambuliaji wote watatu, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Chirwa ambaye humudu
kucheza kama straika na winga.
Post a Comment