STAA wa FC Barcelona,Muargentina,Lionel Messi,na baba yake
Mzazi,Jorge Horacio Messi,wamehukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha miezi 21
baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kulipa kodi inayokadiliwa kufikia €4.1m
(£3.2m;$4.6m) kati ya mwaka 2007 na 2009.
Lakini habari njema ni kwamba wawili hao hatatumikia adhabu hiyo
hiyo ni kutokana sheria za Hispania kusitisha vifungo kwa watuhumiwa
waliohukumiwa adhabu ya chini ya miaka miwili.Pia wakiwa hawana rekodi yoyote
ya makosa kabla ya vifungo husika.
Aidha mahakama hiyo
imewatoza faini kila mmoja kwa kiwango chake.Messi ametakiwa kulipa faini ya
£1.7 huku baba yake Jorge yeye akitakiwa kulipa faini ya £1.3m.
Post a Comment