ZAWADI ya Eid! Wakati leo ikiwa ni siku ya mapumziko katika
sehemu kubwa ya dunia kupisha maadhimisho ya sikukuu ya Eid, klabu za Swansea
City na West Bromwich Albino bado zipo bize kwenye suala lka usajili tayari kwa
kuanza kazi msimu ujao wa Ligi Kuu England.
Swansea City imemsajili beki wa kati wa Uholanzi, Mike van
der Hoorn kutoka Ajax kwa ada ya £2m. Hoorn,23, amesaini mkataba wa miaka
mitatu wa kuitumikia miamba hiyo ya Liberty Stadium na mtihani wake mkubwa
utakuwa ni kupata namba kikosi cha kwanza mbele ya nahodha Ashley Williams,
Federico Fernandez na Jordi Amat.
Hoorn anakuwa mchezaji wa pili toka Uholanzi kujiunga na
Swansea City ndani ya masaa yasiyozidi 48.Wa kwanza alikuwa na Leroy Fer
aliyejiunga na Swansea City jana akitokea QPR kwa ada ya £4.1m.
West Brom imetangaza kumsajili mshambuliaji wa Scotland,Matt
Phillips kutoka Queens Park Rangers kwa ada ya £5m. Phillips,25,amesaini
mkataba wa miaka minne na tayari ameishajiunga na kikosi hicho tayari kwa
maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu England.
Post a Comment