PEP GUARDIOLA amekubali yaishe na kufanya uamuzi wa
kumbakisha kiungo Yaya Toure Manchester City.
Kocha Guardiola amemalizana kwa amani na Yaya Toure kwa
kumwambia kiungo huyo kwamba anahitaji msaada wake na kuigeuza Manchester City
kuwa kama ilivyokuwa Barcelona.
Kiungo huyo amekuwa mchezaji muhimu wa Man City tangu Guardiola alipomruhusu
kuondoka Nou Camp na kutua Etihad kwa dili la Pauni 24 milioni miaka sita
iliyopita, winning two ameshinda mataji ya Ligi Kuu, Kombe la FA na mataji mawili
ya Capital One.
Iliaminika kwamba kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33
angeondoka mara ilipothibitishwa kwamba bosi wake wa zamani wa Barca, ameteuliwa kuwa kocha wa City.
Lakini kocha Guardiola amemhakikishia Yaya Toure atakuwa
kiungo katika mipango yake kwa sababu anajua falsafa ya soka alilolitengeneza
katika klabu ile ya Catalanya.
Chanzo karibu na Yaya
Toure kimesema: “Kitu cha kwanza kwa alichokisema Pep kwa Yaya alimwambia atakuwa
mchezaji wake mkubwa ndani na nje ya
uwanja.
“Yaya ni mchezaji pekee wa City aliyefanya kazi na Pep na
anaweza kuwasaidia wengine katika kikosi
kuelewa staili yake ya uchezaji ambayo atawataka wacheze.
“Yaya alifurahi alipoambiwa kwamba ni sehemu katika mipango
ya kocha. Hakuwahi kuwa na matatizo binafsi na Pep. Kwa kweli, wakati alipokuwa
wakiondoka Barcelona na kujiunga na City, Pep alimwambia kwamba anataka abaki.”
Toure alionekana kuanza kupambana na mahitaji zaidi ya mwili
wake kutokana na uchovu katika Ligi Kuu msimu ulioisha.
Lakini chanzo kiliongeza: “Yaya amekuwa na mapumziko
mazuri katika kipindi cha majira ya joto
na sasa yuko vizuri na tayari kuonesha kwamba bado ni mchezaji mkubwa.
"Labda kuna wakati msimu uliopita kama alikuwa akitaka
kudorora, lakini sasa ameamka kwa mara nyingine na anataka kuutumikia mwaka
wake wa mwisho wa mkataba na City.”
Kabla ya kufikia hatua hiyo, Yaya Toure alikuwa na ofa kibao
kutoka katika Ligi Kuu ya China sambamba na Inter Milan ya Italia ambako
angeweza kuungana na kocha wake wa zamani wa City, Roberto Mancini.
Post a Comment