KAMBI
ya Timu ya Taifa ya Argentina imeendelea kupata mapigo makali makali tangu
ilipochapwa na Chile katika Fainali za Copa America siku kumi zilizopita nchini
Marekani.
Nahodha
Lionel Messi alianza kuishitua dunia kwa kutanzanga kuachana na timu hiyo,akaja
Rais wa chama cha soka,Luis Segura na sasa aliyekuwa Kocha wake Mkuu,Gerardo
Martino,kutangaza kubwaga manyanga kuifundisha timu hiyo kuanzia Jana Jumanne.
Martino,53,amefikia
uamuzi huo kwa kile kinachodaiwa kuwa kocha huyo wa zamani wa Barcelona na
Newell Old Boys hakuwa akipewa sapoti ya kutosha na chama cha soka cha nchi
hiyo AFA.
Imedaiwa
pia Martino alikuwa akifanyishwa kazi bila ya kulipwa mshahara wake.Mpaka
anabwaga manyanga Martino ameripotiwa kuwa hajalipwa mishahara yake kwa kipindi
cha miezi sita sasa.
Sababu
nyingine iliyodaiwa kumbwagisha manyanga Martino ni kwamba licha ya kupewa
jukumu la kuiongoza Argentina katika michuano ya mwaka huu ya Olyimpiki lakini
ameshindwa kupata wachezaji wa kuunda kikosi hicho hii ni baada ya vilabu vya
nchi hiyo vikiongozwa na River Plate pamoja na Boca Juniors kutia ngumu kutoa
ruhusa kwa wachezaji wao kushiriki katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza
kutimua vumbi lake nchini Brazil mwezi hapo Agosti mwaka huu.
Martino
alianza kuinoa Argentina mwaka 2014 baada ya kuisha kwa fainali za kombe la
dunia zilizofanyika nchini Brazil na Ujerumani kuibuka mabingwa kwa kuichapa
Argentina kwa bao 1-0. Akiwa na Argentina,Martino, aliiongoza Albiceleste
kucheza jumla ya michezo 29,akishinda 19,sare 7 na kufungwa mara tatu dhidi ya
Chile na Ecuador.
Post a Comment