KIROHO
safi Yanga imekubali Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kusimamia mechi zake za
kimataifa lakini kwa sharti maalum ambalo TFF lazima itekeleze.
Juzi Alhamisi, Rais wa TFF, Jamal Malinzi,
alitangaza uamuzi huo baada ya kuona Yanga imefanya ndivyo sivyo kwenye mchezo
wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.
Kwa mujibu wa TFF, Yanga ilikiuka baadhi ya
maagizo ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) yaliyowataka kutoruhusu watazamaji
wa mchezo huo kuwa zaidi ya 40,000 kutokana na kutangaza waingie bure.
Akianza kwa kujibu kutolea ufafanuzi juu ya
hilo, Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit, alisema yote yanayozungumzwa na
TFF si ya kweli kwani walifuata kile walichotakiwa kufanya na Caf.
“Msimamizi mkuu wa mchezo ule, Sidio Jose
Mugadza raia wa Msumbiji, alituuliza uwanja una uwezo wa kuchukua watazamaji
wangapi, tukamwambia ni 60,000, akashangaa.
“Akasema kumbe watazamaji wengi wanaweza
kuushuhudia, hivyo tusimamie ulinzi kwani kama hali ya amani haitakuwepo basi
mchezo usingechezwa.
“Tunakubali TFF kusimamia mechi zetu, ila
mpaka sasa tumetumia Sh milioni 180, hivyo TFF watulipe hizo halafu ndipo
waendelee na hicho wanachokitaka pia wawe wanalipa wenyewe gharama za mechi
hizo.
“TFF
wao wanaitafsiri sheria ya kusimamia mechi za timu zake kwa upande mmoja tu
hasa likija suala la mapato wao ndiyo wanajitokeza lakini kwenye gharama hizo
nyingine wanakaa pembeni,” alisema Deusdedit.
Post a Comment