UONGOZI wa Klabu ya Simba
umeshtukia janja ya mahasimu wao Yanga ya kutaka kumsajili beki wake wa
kushoto, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye inadaiwa tayari wameshaanza
kufanya naye mazungumzo ya kutaka kuvunja mkataba, hivyo uongozi huo umeamua
kumuongeza mkataba mwingine.
Tshabalala ni beki
aliyeonyesha uwezo mkubwa msimu uliopita licha ya timu yake kuyumba mara
kadhaa, hali ambayo ilisababisha Yanga ionyeshe nia ya kumsajili na tayari
kulikuwa na taarifa kuwa imeanza mipango rasmi ya kutekeleza jukumu hilo.
Akizungumza na Championi Ijumaa, beki huyo alisema
taarifa za Yanga kumhitaji amezisikia huku akidai kuwa bado ana mkataba na
Simba na tayari wameanza mazungumzo naye ya kumuongezea mkataba mpya ili Yanga
walimpate.
“Mimi ni mchezaji halali wa
Simba na tayari kuna mazungumzo mapya ya kuongeza mkataba mwingine lakini
sijajua utakuwa wa muda gani.
“Moja ya malengo
niliyojiwekea ni kuhakikisha napata nafasi ya kucheza nje ya nchi, hivyo
mtazamo wangu haupo kwenye kutua Yanga wala timu yeyote ya hapa Bongo mara
baada ya kumalizana na Simba nahitaji kucheza nje,” alisema beki huyo.
Post a Comment