Kampuni
ya simu za mikononi ya Vodacom imetoa Sh milioni 6 kudhamini safari ya
mafunzo ya wahariri 30 wa michezo nchini ambao wanakwenda nchini Kenya.
Wahariri
hao kupitia Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa)
ambao wamepata mwaliko kutoka kwa chama cha Kenya (SJAK), watakwenda
jijini Nairobi kwa ziara hiyo ya mafunzo.
Meneja
Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom, Jacqueline Materu amesema: “Tumeona
hii ni fursa njema kusaidia ziara hiyo ambayo itakuwa na faida katika
maendeleo ya tasnia ya habari pamoja na michezo.”
Kwa upande wa Taswa, Makamu Mwenyekiti, Egbert Mkoko aliwashukuru Vodacom kwa udhamini huo ambao alisema wameonyesha undugu wa damu
Post a Comment