Maandamano hayo yalikuja baada ya vifo vya
vijana wawili weusi waliouawa wiki iliyopita na polisi wa kizungu kwa nyakati
tofauti, lakini baada ya tukio hilo, kijana mweusi pia aliwaua askari watano wa
kizungu kabla ya kujeruhi wengine saba kwa bastola aliyokuwa nayo.
Baada ya kufika kituoni hapo, Snoop na The
Game walifanikiwa kufanya mazungumzo na Meya wa Los Angeles, Charlie Beck na
Mkuu wa Polisi wa L.A, Charlie Beck na baada ya hapo kwa pamoja wakaungana
kukemea vitendo hivyo na kuahidi kulifanyia kazi suala hilo.
Nyimbo na maneno mbalimbali ya kupigania haki
kwa amani na kutiana moyo kwa kinachoendelea zilisikika eneo hilo kabla ya
baadaye Snoop ku-post video katika mitandao ya kijamii akiwashukuru
waliojitokeza kuunga mkono zoezi hilo kwa kuonyesha upendo na uchungu kwa
kilichotokea.
Hata hivyo, mastaa wengine wakiwemo John
Legend, Amber Rose, Rihanna, Hillary Clinton, Justin Timberlake, Beyonce, Kim
Kardashian, Drake, Pink, Tyga na wengine wengi walionyesha hisia zao za
kuchoshwa na matukio hayo katika kurasa zao za mitandao ya kijamii kwa kukemea
na kuwatia nguvu watu weusi.
Post a Comment