Mrwanda (kulia) akishangilia bao na Msuva wakati akiichezea Yanga
MSHAMBULIZI wa zamani wa AFC Arusha, Simba na Yanga SC amekamilisha usajili wake wa mwaka mmoja katika timu ya Stand United akitokea Majimaji FC ya Songea, Ruvuma.
Mrwanda aliichezea Majimaji katika mzunguko wa pili msimu uliopita na kufunga magoli 7 amesajiliwa siku chache baada ya aliyekuwa mfungaji namba moja wa timu hiyo, Elius Maguli kujiunga na klabu ya ligi kuu ya kulipwa nchini Omani.
“Ni kweli tumemsajili Mrwanda ambaye alikuwa mchezaji huru akitokea Majimaji. Ni usajili ambao tunaimani utaisaidia timu yetu,” anathibitisha mtu wa ndani wa timu hiyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa yeye si msemaji wa klabu.
“Danny ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa, tunategemea atawasaidia na baadhi ya vijana na kuwapa mbinu za kiuchezaji. Ni mchezaji ambaye Stand itapata msaada wake mkubwa ndani ya uwanja.”

CHANZO: Shafidauda

Post a Comment

 
Top