JUMA |
BEKI wa pembeni
tegemeo wa Yanga, Juma Abdul amewaambia Simba kuwa kama wasipokuwa wavumilivu,
basi watamtimua kocha wao mpya Mcameroon, Joseph Omog.
Omog alitua
kuifundisha timu hiyo wiki moja iliyopita akitokea nyumbani kwao kabla ya
kuanza kibarua cha kukinoa kikosi hicho hivi karibuni.
Akizungumza na
Championi Jumatatu, Abdul alisema Simba itaweza kufanya vizuri ikiwemo kutwaa
ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya miaka miwili, lakini siyo huu.
Abdul alisema
kitu kikubwa kitakachosababisha wao kushindwa kufanya vema ni kutokana na nusu
ya usajili kufanywa na viongozi na siyo kocha mwenyewe.
Aliongeza kuwa,
Yanga ni tofauti na Simba ambayo yenyewe ipo pamoja muda mrefu na usajili
umefanywa kwa mapendekezo ya kocha wao Mholanzi, Hans van Der Pluijm.
"Simba
kupata mafanikio ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwenye msimu huu ni ngumu na
hata kutufunga yenyewe Yanga wasahau kabisa kutokana na timu yetu kuwepo pamoja
muda mrefu.
"Pia hata
usajili wenyewe uliofanywa na timu yetu ni chini ya kocha wetu aliyetoa
mapendekezo ya usajili kwa viongozi na kusajili, lakini wao Simba nusu ya
wachezaji waliosajiliwa Omog amewakuta.
"Hivyo ni
ngumu wao Simba kufanya vizuri na kitu kibaya zaidi kocha atahitajika
kutengeneza mifumo na kombinesheni za wachezaji, hali hiyo itampa ugumu kocha
huyo, hivyo Simba lazima wawe wavumilivu kwa kumpa muda kocha huyo," alisema
Abdul.
Kocha huyo ana
rekodi kubwa kwa Yanga msimu wa 2013/2014 wa Ligi Kuu Bara akiwa na Azam FC kwani
hakufungwa na timu hiyo kongwe zaidi ya kuifunga mzunguko wa kwanza na wa pili
kutoka sare.
Post a Comment