AFYA
ya Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara imezidi kuwa tete na sasa anatarajiwa
kwenda nje ya nchi kwa matibabu zaidi baada ya tatizo lake la jicho kutopata
nafuu.
Manara
anasumbuliwa na ugonjwa wa macho, huku jicho la kushoto likishindwa kufanya
kazi na sasa ameamua kuangalia mbele zaidi.
Akizungumza
na Championi Jumatatu, Manara alisema muda wowote kuanzia leo Jumatatu,
anatarajiwa kwenda kati ya Uturuki, Ujerumani au India kwa ajili ya matibabu
huku akiwaomba Watanzania kumuombea apone haraka.
“Wiki
ijayo, muda wowote kuanzia kesho (leo), nategemea kwenda nje ya nchini kwa
matibabu zaidi. Inaweza kuwa safari ya India, Ujerumani ama Uturuki lakini hiyo
yote itategemeana na majibu nitakayopata kutoka hospitalini. Muhimu ni
Watanzania kuniombea ili niweze kurejea katika hali yangu ya kawaida,” alisema
Manara.
Post a Comment