July 5, 2016 mwimbaji staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz
aliingia kwenye headlines mitandaoni baada ya kupost kwenye Instagram kuhusu
watu kujitokeza kwa wingi kwenye show ambayo imeandaliwa na mpenzi wake wa
zamani Wema Sepetu pamoja na Christian Bella na Idris.
Wema amesema haya “Watu wamekuwa wakiitumia hii beef yetu
kujipatia followers hasa kwenye mitandao yao kwasababu mtu anaweza akatokea
sehemu yoyote na kuanza kunitukana mimi au kumtukana Naseeb akajipatia
followers wa kutosha, kuna muda mimi nilikuwa naogopa kuimba wimbo wa Diamond unapopigwa
naogopa hata kucheza.”
“Nikisikia nyimbo za Naseeb siwezi kuimba inanibidi nikaze
lakini mwisho wa siku najikomoa mimi mwenyewe nikikaa kwenye gari nitaimba kama
utakuwa unakumbuka nilivyoimba mara ya kwanza watu wakashangaa wakawa
wanajiuliza maswali mengi sana, kwasasa hatuko kwenye mapenzi lakini
tunasaidiana kazi kuonesha uzalendo.”
Post a Comment