INAWEZEKANA kocha
mpya wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog akawa amevunja mwiko kwenye suala la
kupokezana gari moja kwa makocha wapya wa timu hiyo baada ya yeye kupewa gari
lingine jipya.
Imeelezwa kwamba Omog aliyesaini mkataba wa
miaka miwili klabuni hapo, yeye amekabidhiwa gari aina ya Honda na kuachana na
Toyota Mark II Grand lililotumiwa awali na makocha saba waliowahi kuinoa Simba.
Kocha wa kwanza kutumia gari hilo alikuwa
Mserbia, Milovan Cirkovic, akafuata Mfaransa, Patrick Liewig, kisha Mtanzania,
Abdallah Kibadeni kabla ya kumilikiwa na Mcroatia, Zdravko Logarusic na baadaye
ikatua kwa Mzambia, Patrick Phiri.
kahemele |
Baada ya hapo likawa mikononi mwa Mserbia,
Goran Kopunovic kabla ya kumuachia Muingereza, Dylan Kerr na mwisho likaenda
kwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Mganda, Jackson Mayanja ambaye bado lipo kwake
mpaka sasa.
Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo
zimethibitisha kuwa gari analoonekana nalo kocha huyo wa zamani wa Azam FC
tangu asaini kandarasi ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka miwili, ndilo
amekabidhiwa kwa kazi zake.
“Kwa sababu Mayanja tulikuwa naye tangu
mwanzo, tumemuachia gari alilokuwa anatumia tangu mwanzo na Omog ametafutiwa
gari jipya,” alisema Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele.
Post a Comment