MSANII wa
Muziki wa Hip Hop, Miraj Ayoub ‘Mas Stanza’ ambaye sasa anatesa na ngoma yake
ya Mwanzo amechekelea baada ya kuona mashabiki wamempokea vizuri.
Mas Stanza anayevutiwa
na kazi za rapa Nash MC, alisema hii ni ngoma yake ya tatu kuachia na anadai
amefurahishwa na namna mashabiki walivyoupokea wimbo huo ambao ameufanya kwenye
studio za Lupaso.
“Nashukuru
Mungu mashabiki wangu wameupokea vizuri wimbo wangu, pia kwa upande wa redio
zile za mkoani ndiyo zinaonekana kuwa mstari wa mbele kuusapoti, sasa hivi
najipanga kwa ajili ya kuanza kufanya video kali itakayonivusha kimataifa,”
alisema Mas Stanza.
Post a Comment