WAZIRI wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewataka viongozi wa timu
zinazoshiriki Ligi Kuu Bara na Daraja la Kwanza kwenda kuangalia vipaji kwenye
Michuano ya Sports Extra Ndondo Cup inayoendelea kwenye Uwanja wa Bandari
uliopo jijini Dar.
Nape ambaye
alikuwa mgeni rasmi kwenye mchezo uliopigwa jana kati ya Goms ambayo ilishinda
mabao 2-0 dhidi ya Buguruni alisema amefurahishwa na namna michuano hiyo
inavyoendeshwa huku akiwasifia wachezaji wa timu hizo kuwa wamekuwa na vipaji
vikubwa.
“Ninayapongeza mashindano kwa kuwa
yanawakutanisha vijana pamoja, naamini yatatoa vipaji vingi niziombe
klabu za ligi kuu na daraja la kwanza kupitia mabenchi yao ya ufundi
waje kuangalia mashindano haya ili wawasajili wachezaji.
Wakati
huohuo kuhusiana na kashfa ya rushwa iliyojitokeza kwenye mechi za mwisho za
Ligi Daraja la Kwanza Bara, Nape alisema: “Serikali tayari imeunda timu kwa
ajili ya kufuatilia hilo na nimekutana na Mkurugenzi wa Takukuru (Valentino
Mlowola) ili kuhakikisha suala hilo linapatiwa jibu mapema, kama serikali
tunataka kukomesha vitendo vya rushwa na kuukata kabisa ule mzizi wake,”
alisema Nape.
Post a Comment