NEYMAR JR yuko kwenye msuguano mkali wa maisha binafsi ndani
ya Barcelona, imebainika.
Mshauri wa karibu wa mchezaji huyo, Wagner Ribeiro, alianza
wiki hii kwa kusema kwamba klabu tatu kubwa zipo tayari kutoa Euro 200 milion
kumnasa Mbrazili huyo.
Klabu hizo ni PSG, Manchester United na Real Madrid zimekuwa
zikihusishwa na Neymar tangu kumalizika
kwa msimu huu.
Na imedaiwa kwamba kuna sakata zito ndani ya kambi ya Barca
ambalo linamhusisha moja kwa moja Neymar.
"Uhusiano kati ya (Lionel) Messi na Neymar siyo mzuri. Messi hakubaliana na
tabia ya Neymar, wakati Mbrazili huyo haoni jinsi atakavyoweza kushinda tuzo ya
Ballon d'Or akiwa na Messi katika timu moja.”
"Pia, uhusiano wake na kocha Luis Enrique ni mbaya
zaidi kuliko ule kati yake na Messi..." kimesema chanzo cha ndani ya
Barcelona.
Kutokana na hali hiyo, inadaiwa kuwa Neymar ataondoka
Barcelona na kuna dalili kubwa kwamba hilo linaweza kutokea kwenye dirisha hili
la uhamisho wa majira ya kiangazi.
Pamoja na PSG na Manchester United, Real Madrid imetajwa
kuwa kwenye mpango wa kuinasa saini ya fowadi huyo na kuwatishia wapinzani wao
hao kwamba, watarudia kile walichowahi kukifanya kwa Luis Figo.
Barcelona yenyewe bado inaamini Neymar atasaini mkataba mpya
na kuendelea kubaki kwenye kikosi chao na kuachana na vurugu zote kutoka kwa
klabu mbalimbali.
Hata hivyo, inasemwa kuwa jambo hilo si rahisi kama ambavyo
Barcelona inavyotarajia.
Wakati giza kuhusu hatima ya staa huyo likiwa kubwa, dada wa
staa huyo, mrembo Rafaella amezua utata na kuchochea uvumi kwamba, Neymar
ataihama Barcelona kwenye dirisha hili.
Wawakilishi wa klabu za Man United, Real Madrid na PSG
wanaripotiwa kukutana na Mbrazili huyo nyumbani kwao Brazil.
Mrembo Rafaella, ambaye ni dada wa Neymar aliweka picha
kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika maneno ambayo yalichochea uvumi
kuhusu fowadi huyo.
Raffaela aliweka picha ya milango miwili ya treni
iliyokaribiana sana na kisha kuandika maneno: "Natumaini utakwenda mahali
ambako patakufanya uwe na furaha."
Post a Comment