WIKI iliyopita Mkuu wa Idara
ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, alitangaza kuendelea kupiga kazi
kama kawaida na kwamba hatambui adhabu yake ya kufungiwa mwaka mmoja aliyopewa
na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwani hajapewa barua
ya hukumu yake, hata hivyo TFF imemwambia asithubutu kwani kama ni barua ya
adhabu alishakabidhiwa.
Muro, juzi Ijumaa kwenye
vyombo vya habari alisema alikuwa likizo na si kutumikia kifungo hicho
alichopewa baada ya kukutwa na hatia ya kupingana na maamuzi ya TFF pamoja na
kutakiwa kulipa faini ya milioni tatu.
Katibu wa TFF, Selestine
Mwesigwa, amesema Muro anajua nini kitamtokea iwapo atathubutu kufanya kazi kwa
sasa kutokana na adhabu inayomtaka kutojihusisha na soka mwaka mzima.
“Yeye anaongea lakini
hajatuletea tamko lake rasmi na ataongea hukohuko, lakini kwetu tunatambua
adhabu iko palepale,” alisema katibu huyo.
Alipoulizwa iwapo Muro
ataanza kazi itakuwaje, Mwesigwa alisema: “Siwezi kusemea tuhuma za ‘kama’
lakini ieleweke iwapo ikitokea, nadhani anajua adhabu yake na kwa kuwa
halijatokea (kufanya kazi kama alivyotamba) tuliache kwanza.”
Katibu huyo wa zamani wa
Yanga, alisema Muro alipewa barua ya hukumu ambayo nakala yake ipo kwa waajiri
wake, Klabu ya Yanga ambayo ilitumwa kwa katibu, Baraka Deusdedit.



Post a Comment