BAADA kupata sare inayodaiwa kuwa ni ya mbeleko dhidi ya African Lyon, Kocha Mkuu wa Azam, Mhispania, Zeben Hernandez, amekiri kuwa kikosi chake kina upungufu mkubwa katika safu ya ushambuliaji na kwamba anahitaji mtu sahihi wa kucheza nafasi hiyo.
Katika mchezo huo uliopigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa  Azam complex, Azam ilipata bao la kusawazisha katika dakika sita za nyongeza baada ya kumalizika dakika tisini ikiwa inaufukuza mchezo kwa 1-0.

 “Ni kweli ufungaji katika kikosi changu umekuwa ni mgumu, ni kwa sababu bado safu hiyo ina upungufu wa  washambuliaji, ingawa ninachokifanya kwa sasa ni kuwatumia hawa waliopo kwa sababu suala hilo mpaka uongozi wa klabu unalijua.

“Lakini kwa sasa nina mambo mawili tu ya kufanya, aidha kuwatengeneza wachezaji waliopo ili waweze kucheza vizuri katika nafasi hiyo ama kuangalia uwezekano wa kutafuta straika mpya kabisa,” alisema Zeben.

Post a Comment

 
Top