KUNGO wa Manchester United, Ander Herrera amesema kuwa safari hii hawatafanya utani na badala yake wataichukulia michuano ya Europa League kwa umakini mkubwa tofauti na ilivyokuwa awali.

Man United ipo katika michuano hiyo kutokana na kumaliza msimu katika Premier League ikiwa katika nafasi ya tano huku ikiwa na kumbukumbu mbaya ya michuano hiyo.


Man United ilitolewa na Athletic Bilbao katika hatua ya 16 Bora mwaka 2012 pia msimu uliopita ilitolewa na Liverpool katika hatua hiyohiyo.

"Nafikiri ni michuano mizuri na tunataka kushinda, Europa League imekuwa michuano muhimu kila msimu na imepata umaarufu.


“Sisi ni klabu kubwa na tunaheshimu wapinzani wetu lakini tutapambana ili tuwe mabingwa, tuna kikosi kizuri, tunao wachezaji wanaoweza kucheza Alhamisi, Jumapili, Alhamisi na Jumapili tena,” alisema Herrera.

Post a Comment

 
Top