STRAIKA Mtanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji katika Klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta amezidi kung’aa baada ya usiku wa kuamkia leo kuifungia timu yake mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Lokeren katika mchezo wa ligi kuu nchini humo.

Samatta ambaye amejiunga na kikosi hicho msimu huu akitokea TP Mazembe ya DR Congo, aliifungia timu hiyo mabao katika dakika ya 34 na 39 akipokea astisti kutoka kwa Alejandro Pozuelo, bao jingine la Genk lilifungwa na Leon Bailey (48).

Post a Comment

 
Top