AVEVA KUSHOTO AKIKABIDHIWA HUNDI NA MO DEWJI KWA AJILI YA USAJILI WA WACHEZAJI WA SIMBA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), inaendelea kumchunguza Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi.

Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba, alisema uchunguzi dhidi ya Rais huyo wa Simba na viongozi wenzake bado haujakamilika hadi hivi sasa na kwamba suala hilo likikamilika watatoa taarifa rasmi.

Alisema uchunguzi huchukua muda mrefu hivyo suala la kumfikisha mahakamani Rais huyo bado hadi pale kila kitu kitakapokamilika.

“Uchunguzi unachukua muda mrefu hadi mtuhumiwa kufikishwa mahakamani kwani si kitu cha siku mbili au tatu, hivyo mambo hayo yakikamilika tutatoa taarifa,” alisema Misalaba.

Post a Comment

 
Top