April 6, 2025 11:46:17 AM Menu




HOFU! Siku moja baada ya kutangaza kuwa Katibu wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, Mzee Akilimali ameibiwa baraghashia tayari imeripotiwa kofia hiyo imepatikana.
Tukio hilo inadaiwa lilitokea juzi Asubuhi Mzee Akilimali alipokuwa Mtoni Mtongani jijini Dar alipokwenda kumtembelea Mzee Mwika ambaye ni rafiki yake.
 Akizungumza jijini Dar Mzee Akilimali alisema anashukuru Mungu kuipata kofia hiyo na kwamba vibaka ndio waliomuibia ambao wanaripotiwa kuwa tayari walishaiuza.
Anasema baada ya kuibiwa wala hakuwa na hofu kwa kuwa wenyeji wake walimuahidi kuitafuta mpaka kuipata kwa kuwa wanafahamu sehemu wanayouza vitu vya uwizi.
Imeripotiwa kuwa kijana mmoja aliyeiba alikamatwa na kupewa kipigo kikali kabla ya kufikishwa kituo cha Polisi Mtoni Mtongani.
24 Aug 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top