UONGOZI wa Simba umesema hauna mpango wa kumuuza beki wao wa kati Mganda, Juuko Murshid licha ya kuwa mchezaji huyo amekuwa akikabiliwa na ushindani wa namba tangu kuanza kwa msimu huu.

Juuko alipewa jina la Beki Jasiri na mashabiki wa timu hiyo kutokana na aina ya uchezaji wake wa kupambana mwanzo mwisho, ilitajwa kuwa anaweza kuuzwa Uarabuni au Afrika Kusini.

Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Simba, Said Tully, amesema ni mapema kumuuza mchezaji hivi sasa, kwani ndiyo kwanza wanatengeneza timu ya ushindani.

“Kwanza hatujapokea ofa kutoka kwenye klabu yoyote ikimuhitaji Juuko, tunataka kuendelea kuwa na kikosi kipana ili ushindani uwe mkali,” alisema Tully.

Post a Comment

 
Top