KIKOSI CHA SIMBA KINACHOANZA LEO V  JKT RUVU
DAK 2: simba wanaonekana kumiliki mpira hususan eneo la kiungo na JKT wanaonekana kuzuia muda mwingi


Dk 7: JKT Ruvu wanaonekana kuamka sasa na wanafika langoni mwa  wapinzani wao. Simba inaonekaana kutokuwa makini zaidi hasa wanapolifikia lango la wapinzani wao huku wkaipoteza mipira mingi nje ya 18.
 

DK 13 Mavugo anafanyiwa faulo nje kidogo ya 18, na anapiga mwenyewe faulo hiyo lakini shuti lake linapaa kidogo nje ya lango la JKT Ruvu



Mchezaji wa JKT Ruvu anashindwa kufunga  bao la wazi kabisa kufuatia  kumpiga chenga kipa na kisha lango kubaki na mabeki wa Simba ambao wameokoa. Mechi bao 0-0
 

Dk 22. Kichuya almanusura awape Simba bao la kuongoza kutokana na shuti lake kali alilopiga nje ya 18 kupanguliwa kiufundi na kipa wa JKT na kuwa kona ambayo haijazaa matunda



Dk 35: Kichuya anawapiga chenga mabeki watatu wa JKT ndani ya 18 akitaka kwenda kufunga lakini hata hivyo chelewachelewa yake inawafanya mabeki wa maafande hao wamuwahi na kuutoia mpira kwenye hatari.

DK 45; za kipindi cha kwanza zimemalizika Simba 0-0 JKT Ruvu
punde tutawaletea uchambuzi wetu  

 Kipindi cha pili kimeanza



Dk 51: Jamal Mnyate anatoka anaingia Miwnyi Kazimoto



DK 65: Anatoka Blagnon anaingia Ajib





Simba wanaonekana kusaka bao kwa nguvu lakini kila wanapolikaribia lango la wapinzani wamekuwa wakishindwa kujipanga vyema



JKT sasa wanaonekana kucheza pasi za kugongeana 


DK 70 Offside MAvugo.

Ajib tangu alivyoingia naaonekana kuitesa vilivyo safu ya mabeki wa JKT


DK 90+4 SIMBA 0-0 JKT

FULL TIME SIMBA 0-0 JKT RUVU
 


UCHAMBUZI DK 45 ZA AWALI

Simba ambayo inaongozwa na Joseph Omog kwenye benchi, inaonekana kucheza mpira wa pasi lakini tatizo ambalo lipo wazi kabisa ni kushindwa kuzitumia nafasi wanazopata na kingine ambacho ni kikubwa zaidi ni washambuliaji wake kushindwa kutengeneza njia mbadala ya kuwapita mabeki wa timu pinzani.



Mara nyingi wanapofika langoni kwa JKT wamekuwa kama hawajui wafanyaje na kujikuta wakitumia muda mwingi kurudidisha mipira nyuma au wananyang’anywa, washambuliaji wanatakiwa kuwa na plan B kwani ni kama wameshikwa au wanagandishwa kila wanapolifikia lango la wapinzani wao. Upande wa mabeki unaonekana kutulia sana.



JKT RUVU

Inacheza vizuri lakini wanaonekana kutaka kupiga pasi nyingi zaidi kwa lengo la kushindana na Simba na hilo linaweza kuwagharimu. Walipata nafasi moja nzuri ambayo kama wangeitumia ipasavyo basi sasa wangekuwa wana bao moja lakini kutokana na mpigaji kutokuwa makini katika umaliziaji ulisababisha mpira uokolewe na mabeki wa Simba.



ILIKUWA HIVI; Mshambuliaji wa JKT alitanguliziwa mpira na mwenzake ambapo alionekana kuwazidi mabeki wote wa Simba na wakati huo Angban akawa ametoka kusaidia na kweli akaugusa mpira ambao pia ukarudi kwa mchezaji mwingine wa Maafande hao ambaye aliutuliza lakini akashindwa kupiga kiufundi kwani mpira ulitua miguu kwa beki wa Simba ambaye aliuosha mbele, kumbuka wakati huo Angban alikuwa bado yupo chini.


 
 

Post a Comment

 
Top