KOCHA Joseph Omog amesema bado uelewano wa uwanjani kati ya Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib haujakaa sawa kimbinu, hasa katika kufunga.

“Bado tuna tatizo katika kufunga mabao na sipendezwi na namna Mavugo na wenzake wanavyocheza kwa sababu wanachelewesha ushindi wetu kwa sababu wanakosa utulivu wanapokuwa mbele ya lango la wapinzani wetu na kujikuta wakikosa mabao mengi ya wazi tofauti na nafasi ambazo wanazitengeneza.

“Tayari nimeshaliona tatizo hilo mara baada ya mchezo wetu wa kwanza na nitalifanyia kazi kabla ya michezo ijayo ya ligi.

“Nimeshaandaa mazoezi maalumu yatakayokuwa ya kufunga tu ambayo naamini wakiyaelewa, basi tutakuwa tunashinda idadi kubwa ya mabao tofauti na ambayo tunayapata sasa,” alisema Omog.  

Post a Comment

 
Top