BEKI na nahodha wa zamani wa Arsenal, Tony Adams amesema hana wasiwasi na hali ya klabu yake kuanza kwa mwendo wa taratibu katika msimu huu mpya na anaamini matokeo mabaya hayatokani na kutosajili kwa fedha nyingi.

 Arsenal ina pointi moja katika michezo miwili ya Premier League ikiwa imeshapoteza mechi dhidi ya Liverpool na kupata suluhu dhidi ya Leicester City.

Adams ambaye ni mkurugenzi wa soka katika moja ya timu inayoshiriki ligi ya China, amesema mashabiki hawatakiwi kuwa na papara ya kutaka kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger atumie fedha nyingi kusajili.

"Kuna wachezaji wengi walikuwa nje, kupata pointi moja dhidi ya mabingwa, wiki iliyopita yalikuwa ni matokeo mazuri," alisema Adams na kuendelea:

“Matokeo mabaya katika mechi za kwanza ni kawaida, bado naunga mkono falsafa za Wenger za kutotumia fedha nyingi kusajili japokuwa nahisi anatakiwa ‘aibalansi’ timu hasa katika safu ya ulinzi na ushambuliaji."

Post a Comment

 
Top