NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi na Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Angelina Mabula ameahidi kutoa Sh 50,000 kila bao litakalofungwa na kikosi cha Mbao katika michezo yote iliyobaki ya Ligi Kuu Bara msimu huu.

Mbao ambayo makao yake makuu ni Ilemela, ilifanikiwa kutoka sare ugenini dhidi ya Stand United katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu kabla ya wikiendi iliyopita kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC.

Mabula alisema licha ya Mbao kupoteza mchezo huo lakini alifurahishwa na kiwango walichokionesha katika mchezo huo kwani walitengeneza nafasi nyingi tofauti na wapinzani wao jambo ambalo limemvutia kununua kila bao watakalofunga timu hiyo michezo iliyobaki.
 
Waziri Angelina Mabula katikati
"Ukweli timu yetu imepoteza mchezo katika uwanja wake wa nyumbani (Kirumba) lakini nimefurahishwa na kiwango ambacho vijana wamekionesha dhidi ya Mwadui,

hili limenifanya nihamasike kununua kila bao watakalofunga katika mechi zijazo kwa Sh 50,000 ili kuhamasisha vijana wetu kujiamini na kuisaidia timu kupata matokeo mazuri,” alisema Mabula.

Post a Comment

 
Top