SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeitolea nje Klabu ya Azam kutumia uwanja wao wa Azam Complex kucheza na Simba na Yanga katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Azam waliwasilisha barua TFF ya kuomba kuanza msimu huu kwa kutumia uwanja huo kucheza mechi ya nyumbani dhidi ya timu hizo mbili badala ya ule ya Taifa na Uhuru,  jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na BINGWA jana, Ofisa Habari wa Azam, Jafari Iddi, alisema shirikisho hilo limekataa ombi lao kwa sababu za kiusalama.
Jafari alisema kufuatia majibu hayo, wanatarajia kukutana keshokutwa baada ya mchezo wao dhidi ya Majimaji kwa lengo la kujadili suala hilo.
“Baada ya mechi yetu dhidi ya Majimaji, tutajua kabla ya kukutana na Simba.
“Juzi mmeona Serengeti Boys wakicheza hapa mechi ya kimataifa, sasa iweje ishindikane hizi za Simba na Yanga,” alisema Jafari.

Post a Comment

 
Top