KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog, raia wa
Cameroon, amesema kikosi chake kipo kamili kwa
ajili ya mchezo wao wa leo Jumamosi dhidi ya
Maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu,
hivyo wapinzani wake hao watamsamehe kwani
tayari amewaandalia kipigo.

Simba iliyoanza msimu huu wa Ligi Kuu Bara kwa
ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda, leo itacheza
 na ‘wajeda’ hao kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

Omog ameliambia gazeti hili kuwa, lengo lake ni
kuona kikosi chake kinashinda katika kila mchezo
wa ligi na kukusanya pointi nyingi ambazo zitakuja
kuwabeba hapo baadaye katika kuwania ubingwa
wa ligi hiyo.
“Tunataka kuwa mabingwa, kila siku nasema hivi na
watu wamekuwa kama hawaamini, ili kudhihirisha hilo, 
tumeanza kwa ushindi kwenye mchezo wa kwanza,
 tunaenda tena mchezo wa pili kushinda.

“Huwezi kuwa bingwa bila ya kushinda mechi nyingi, 
tumedhamiria kupata pointi tatu kwenye kila mchezo
wetu, hivyo JKT Ruvu watatusamehe tu kwani lazima 
tuwafunge. Najua na wao wamejiandaa kama sisi,
lakini hilo halituzuii kushindwa kuwafunga kwa
sababu tuna kikosi imara na wachezaji wenye
uwezo kuliko wao,” alisema Omog.

Post a Comment

 
Top