MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amiss Tambwe, ameanza kumgwaya Laudit Mavugo wa Simba kutokana na mpira mwingi aliocheza juzi wakati wakishinda mabao 3-1 dhidi ya Ndanda, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mavugo ameonekana kumuibua Tambwe baada ya kusema msimu huu wa Ligi Kuu wanaweza kufanya vibaya kutokana na uchovu wa kucheza michezo mingi bila kupumzika.
Yanga wanashiriki hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo wanatarajia kucheza na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC) katika mchezo wa marudiano utakaochezwa wiki hii, mjini Lubumbashi.

Akizungumza jana kabla ya kuondoka, Tambwe alisema msimu wa ligi uliopita wachezaji Yanga walikuwa na kibarua kigumu cha kutetea taji lao na hawajapumzika, kwani wameunganisha mechi za kimataifa.
“Uchovu unaweza kutusumbua, kama utakumbuka tangu tumemaliza ligi tumekuwa katika mashindano ya kimataifa kwa muda mrefu bila kupumzika, tuna kazi kubwa mbeleni,” alisema Tambwe.
Tambwe alisema pamoja na uchovu mkubwa walionao wachezaji wenzake, lakini wamejipanga vya kutosha kuhakikisha wanatetea ubingwa wao.

Post a Comment

 
Top