KIUNGO mpya kipenzi cha mashabiki wa Simba, Shiza Kichuya, amesema kamwe hawezi kukaa  benchi katika kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Joseph Omog.
Kichuya, aliyejiunga na Simba na msimu huu  kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mtibwa Sugar, anaamini ataepukana na benchi kutokana na jitihada zake uwanjani.
Alisema ni vigumu kwake kukutana na balaa la kusugua benchi kwavile anafahamu siri ya kuepukana nalo ambayo ni kuwa na nidhamu ndani na nje ya uwanja.
“Binafsi naamini vitu vyote muhimu ambavyo vinanipa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza ninavyo, lakini pia natimiza majukumu yangu ipasavyo, hivyo naanzaje kukaa benchi hapa,” alisema.
Tangu kutua katika kikosi hicho, Kichuya amekuwa akionyesha kiwango cha hali ya juu kiasi cha kujihakikishia namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Kocha Omog.

Post a Comment

 
Top