Mtangazaji mkongwe katika tasnia ya burudani Bongo, Salama Jabir, amefunguka na kudai kuwa aliwahi kununiwa kitambo kirefu na rapa Mwana FA kipindi hicho, kisa alimsema baada ya rapa huyo kuvaa shati ambayo hakuipiga pasi kwenye video ya lililokuwa kundi lao East Cost team.
Akizungumza kupitia kipindi cha The Playlist cha Times fm jumamosi iliyopita, Salama amedai ni kweli Mwana FA hakuwa amenyoosha pasi kwenye video hiyo ambayo haikumbuki hata hivyo.
“Basi tulikutana Moroco pale nakumbuka kwenye mataa, AY akafungua kioo kidogo pembeni yake alikuwapo Mwana FA, nikawasalimia ila FA akanipotezea, sasa baadae namuuliza AY ananiambia eti Binamu kanikazia kisa nimesema hakunyoosha shati.
“Lakini mwenyewe anakiri ni kweli hakuwa amepiga pasi, mimi nilikuwa nafanya kazi yangu, sikuwa nafanya vile nnavyopenda au kama bifu No” Alisema.
CHANZO: timesfm

Post a Comment

 
Top